Na Yusuph Mazimu, BBC Swahili
Mjadala umeendelea kuwa mkubwa nchini Tanzania kuhusu suala la bandari. Umedumu kwa zaidi ya mwezi mmoja na unaweza kuwa kuwa moja ya mijadala mirefu na iliyodumu kwa muda mrefu zaidi nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.Na hauonekani kumalizika katika majuma ya karibuni. Inaonekana dhahiri utaendelea kwa muda na kila litakapotajwa ama kutokea jambo lolote linalohusu bandari mjadala utaibuka na kushika kasi tena.Mjadala huu unatokana na uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuingia mkataba na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari za bahari na maziwa Tanzania.Mkataba huu unaofahamika kwa lugha ya Kiingereza kama Inter-Governmental Agreement-IGA na wenye ibara 31, uliingiwa mnamo Oktoba 25, 2022, kabla ya kuridhiwa na Bunge la nchi hiyo Juni 10, 2023 kupitia Azamio la Bunge.
Full article link: https://www.bbc.com/swahili/articles/czv1yjkrq0do