Na Yusuph Mazimu, BBC
Kwa wengi njiwa ni kitoweo na hufugwa kwa mapenzi si biashara. Lakini Deogratius Temba, kijana kutoka Dodoma, Tanzania amebadilisha dhana hiyo. Anafuga njiwa wa kipee.Hawa ni njiwa wanaojulikana kama njiwa wa mapambo ambao hutumika kupendezesha makazi, maofisi ama sehemu zingine kama mahoteli na za kupumzikia. Kati zaidi ya aina 10 ya njiwa wa mapambo alionao Deogratius, mmoja anauzwa kati ya dola $85 mpaka $180 au shilingi laki 4 za Tanzania.Unaweza kujiuliza wanafananaje njiwa hawa, na kwanini kijana huyu maarufu kama Deo Manjiwa ameamua kuwafuga njiwa hawa wa mapambo? Mwandishi wetu Yusuph Mazimu alimtembelea huko Dodoma kujua mengi.
Full article link: https://www.bbc.com/swahili/articles/cn0elemnk6xo