Na Yusuph Mazimu, BBC
Mamilioni ya watu duniani hupoteza maisha kwa sababu ya magonjwa ya moyo, saratani na uzee. Kwa ugonjwa wa saratani pekee, Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria kuwa kufikia mwaka 2030 utapoteza maisha ya watu zaidi ya 1.1milioni barani Afrika kama hautadhibitiwa.Lakini sasa huenda idadi ya vifo hivyo na vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na uzee ikapungua kwa matumizi ya mtama hasa wa kahawia. Kituo cha Utafiti wa kilimo, TARI-Ilonga, nchini Tanzania kimegundua mbegu za mtama 'inayoweza kupunguza magonjwa kama ya saratani, kisukari, magonjwa ya moyo na kupunguza kasi ya uzee'. Mwandishi wetu Yusuph Mazimu ametuandalia taarifa ifuatayo.
Full article link: https://www.bbc.com/swahili/articles/cd1gk4wx538o