Na Yusuph Mazimu, BBC
Wanawake katika mkoa wa Kigoma magharibi mwa Tanzania wanalazimika kuyatoroka makaazi yao kutokana na hofu ya visa vya ubakaji vinavyodaiwa kutekelezwa na kundi linalojulikana kama 'teleza'.Mashirika ya kiraia yanaeleza kuwa kumeshuhudiwa visa 43 vinavyojulikana vya wanawake kubakwa tangu 2016 mpaka April mwaka huu.Hatahivyo yanashutumu kwamba hatua madhubuti hazijachukuliwa kukabiliana na visa hivyo.Polisi nchini inaeleza kwamba washukiwa kadhaa wamekamatwa.Lakini je 'teleza' ni kina nani na ni kwanini wanawabaka wanawake?'Teleza' kama wanavyofahamika, inaarifiwa ni kundi la vijana wanaodaiwa kutokuwa na shughuli.Jina hilo limetokana na mtindo wao maarufu wanaotumia wa kujipaka mafuta machafu meusi katika miili yao kuepuka kutambulika na pia kuwasidia kushopoka kwa kuteleza wanapojaribu kukamatwa.
Full article link: https://www.bbc.com/swahili/habari-48578619